PUTIN ASIFU UHUSIANO NA CHINA WAKATI WA KUANZA KWA MAZUNGUMZO YAO

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wameanza mazungumzo ya pande mbili mjini Beijing, mkesha wa sherehe ya gwaride kubwa la kijeshi katika mji mkuu wa China.

Putin alipongeza uhusiano kati ya nchi hizo, akisema uko katika "kiwango cha kipekee".

"Rafiki mpendwa, mimi na wajumbe wote wa Urusi tunafurahi kukutana tena na marafiki na wafanyakazi wenzetu wa China," Putin alimwambia Xi, kulingana na video iliyochapishwa kwenye Telegram katika akaunti rasmi ya Urusi.

"Mawasiliano yetu ya karibu yanaonyesha hali ya kimkakati ya uhusiano wa Urusi na China, ambao uko katika kiwango cha juu sana," aliongeza.

"Siku zote tulikuwa pamoja wakati huo, na bado tuko pamoja hadi sasa."

Xi alimwambia Putin kwamba "uhusiano kati ya China na Urusi umestahimili jaribio la mabadiliko ya kimataifa" - akiongeza kuwa Beijing iko tayari kufanya kazi na Moscow "kukuza ujenzi wa mfumo wa utawala wa kimataifa wenye haki na busara".

Xi anatazamiwa kuwa mwenyeji wa gwaride kubwa zaidi la kijeshi nchini China siku ya Jumatano, ambalo litaadhimisha miaka 80 tangu Wajapani walipojisalimisha nchini China mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia.

Share: