Prof. adolf mkenda: mabadiliko makubwa ya mitaala yameanza mwaka huu 2024

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema “Mabadiliko makubwa ya Mitaala yameanza Mwaka huu (2024) yakihusisha ngazi ya Darasa la Kwanza na la Tatu, upande wa Sekondari tumeanzia Kidato cha Kwanza kwa Shule za Mkondo wa Amali. Pia, mabadiliko yatahusisha Kidato cha Tano na Vyuo vya Ualimu”

Ameeleza mabadiliko hayo ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 ambayo inabainisha mwisho wa Elimu ya Msingi ni Darasa la Sita

Ameongeza “Wanafunzi wa Darasa la Tatu kwa sasa ikifika Mwaka 2027 watakuwa Darasa la Sita na ndio mwisho, wale wa Darasa la Nne la sasa wao watakuwa Darasa la Saba la mwisho kwa Mtaala wa zamani.”

Share: