Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma imeanzisha uchunguzi wa jinai.
Polisi nchini Bolivia wamemkamata kiongozi wa jaribio la mapinduzi, saa chache baada ya ikulu ya rais katika mji mkuu La Paz kuvamiwa na wanajeshi.
Wanajeshi walikuwa wameshika doria kwenye Murillo Square ambapo majengo muhimu ya serikali yanapatikana. Wote walijiondoa baadaye.
Kiongozi wa waasi, Jenerali Juan José Zúñiga, alikuwa amesema anataka "kurekebisha demokrasia" na kwamba ingawa anamheshimu Rais Luis Arce kwa sasa, kutakuwa na mabadiliko ya serikali. Sasa yuko chini ya ulinzi.
Rais Arce alilaani jaribio hilo la mapinduzi, akitoa wito kwa umma "kujipanga na kuhamasisha... kwa ajili ya demokrasia".
"Hatuwezi kuruhusu kwa mara nyingine tena majaribio ya mapinduzi kuchukua maisha ya watu wa Bolivia," alisema katika hotuba taifa kupitia televisheni kutoka ikulu ya rais.
Maneno yake yalijitokeza wazi, huku waandamanaji wanaounga mkono demokrasia wakiingia mitaani kuunga mkono serikali.
Maneno yake yalijitokeza wazi, huku waandamanaji wanaounga mkono demokrasia wakiingia mitaani kuunga mkono serikali.
Bw Arce pia alitangaza kuwa anateua makamanda wapya wa kijeshi, na kuthibitisha ripoti kwamba Jenerali Zúñiga amefukuzwa kazi baada ya kumkosoa waziwazi kiongozi wa zamani wa Bolivia, Evo Morales.
Bw Morales pia alilaani jaribio la mapinduzi na kutaka mashtaka ya jinai kuanzishwa dhidi ya Jenerali Zúñiga na "wasaidizi wake".
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma imeanzisha uchunguzi wa jinai.