Pepsi ilimiliki vifaa vya jeshi la urusi baada ya nchi kushindwa kulipa deni

Mwanzoni mwa Miaka ya 1990 Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi Ilikuwa Inamiliki Vifaa Vingi vya Kijeshi Kama Manowari 17, Mashua, Meli za Kijeshi na Vilipuzi vya Kijeshi. Miaka ya 1950 Urusi Ilihitaji Pepsi Ikajenge Viwanda wa Soda Urusi kwa Malipo, Waliposhindwa Kulipa Pesa Ndipo Wakalipa Vifaa vya Kijeshi.

Mwaka 1959 US kwa kupitia makamu wa Rais Richard Nixon walitembelea Urusi na kukutana na Kiongozi wa Urusi Khushchev, huko walikubaliana kuwa waingia mkataba ambao US italipwa kwa kufanya uwekezaji wa viwanda vya Pepsi nchini humo.

Muda wa malipo ulipofika wakabutwalika baada ya kugundua kuwa kumbe pesa ya Urusi (Ruble) haipo kabisa katika mbadilishano wa pesa kimataifa, yaani ukiwa na ruble huwezi exchange na pesa yoyote duniani husuani Dollar, hivyo malipo yakawa magumu.

Basi kuona hivyo ilibidi Urusi wailipe Pepsi kinywaji cha Vodka. Yani ilikuwa Pepsi anachukua Vodka Urusi na anaenda kuiuza US kama ndio malipo sasa.

Ruble ni pesa ya Urusi kama ilivyo Shillingi, Dollar, Pound au Rupia. Kwahivyo miaka hio hii Ruble ilikuwa inatumika Urusi tuu, huwezi kufanya exchange na pesa yoyote ya nje.


Kufika mwaka 1989 uzalishwaji wa pombe hii maarufu ya Urusi (Vodka) ukashuka, na kumbuka Pepsi nao wana mkataba wao kwamba kutokana na uwekezaji walioufanya basi Urusi inawalipa hizo Vodka baada ya mfumo wa pesa kuwa mgumu.

Baada ya uzalishwaji wa Vodka kuwa finyu ndipo mwaka huo 1989 wakaingia makubaliano mengine ya kulipa vyombo hivyo vya kijeshi mpaka mkataba ulipomalizika, na pepsi walikubali kwakua waliona ni njia pekee ya kuendelea kuuza Pepsi nchini Urusi.

Share: