Paul kagame ameshinda tena kiti cha urais baada ya kupata asilimia 99.15 ya kura zote

Mgombea Urais wa Chama cha RFP, Paul Kagame ameshinda tena kiti hicho baada ya kupata kura 7,099,810 sawa na asilimia 99.15 ya kura zote zilizopigwa ambazoni 9,071,157.

Kagame amewashinda Frank Habineza wa Chama cha Democratic Green aliyepata jumla ya kura 38,301 sawa na asilimia 0.53 na Phillipe Mpayimana aliyepata kura 22,753 sawa na asilimia 0.32.

Wananchi wa Rwanda, Julai 15, 2024, wamepiga kura katika Uchaguzi Mkuu wao ikiwa ni mara ya nne tangu yatokee mauaji ya kimbari mwaka 1994. Kura za ubunge zinaendelea kuhesabiwa.

Share: