Papua new guinea haina makubaliano ya usalama na china

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea amesema hakujawahi kufanyika mazungumzo ya masuala ya ulinzi na China, baada ya taifa hilo lenye utajiri wa rasilimali kusaini makubaliano ya usalama na jirani yake, Australia.

James Marape alisema siku ya Jumapili (Disemba 10) kwamba nchi yake imekuwa ikifanya mambo yake kwa uwazi, na kwamba alipoitembelea Beijing mwaka huu akiwa na mawaziri yake, hakikuwa na mazungumzo yoyote kuhusiana na mambo ya ulinzi na usalama.

Kwenye mkutano wake na wawekezaji mjini Sydney, kiongozi huyo wa New Papua Guinea alisema uhusiano wao na China ni masuala ya kiuchumi. Mnamo mwezi Mei, nchi hiyo ilisaini makubaliano ya ulinzi wa nje na Marekani, na wiki iliyopita ikafikia makubaliano ya usalama wa ndani na Australia.

Share: