Papa francis aomboleza vifo vya "raia wasio na ulinzi" gaza

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na mauaji yaliyoripotiwa ya wanawake wawili Wakristo ambao walikuwa wametafuta hifadhi katika majengo ya kanisa kabla ya kuuawa.

Katika hotuba yake ya kila wiki, kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ameeleza kuwa "raia wasio na ulinzi" wanalengwa kwa kupigwa risasi na kushambuliwa kwa mabomu.

Ameendelea kueleza kuwa, wanawake hao waliuawa na "wadunguaji" na kwamba nyumba ya watawa iliyoanzishwa na Mama Teresa pia iliharibiwa na makombora ya Israel.

Papa Francis pia ametoa wito wa kusitisha mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas uliozuka tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kufanya shambulio ndani ya ardhi ya Israel.

Share: