Pac yapitia taarifa ya ukaguzi wa ufanisi wa utoaji wa huduma za afya

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe Naghenjwa Kaboyoka imepitia na kuchambua taarifa ya ukaguzi wa ufanisi katika udhibiti wa utoaji wa huduma za afya kwenye vituo binafsi na vya hiari.

Kamati hiyo pia imepitia na kuchambua taarifa ya ukaguzi wa kiufundi kuhusu ujenzi wa Shule za Sekondari kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP).

Kikao hicho kimefanyika leo katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila.

Share: