Ni mara ya 4 kwa Migomo kutokea nchini humo tangu Rais Bola Tinubu alipochaguliwa kuongoza Taifa hilo linaloripotiwa kukabiliwa na mgogoro wa Kiuchumi
Vyama na Umoja wa Wafanyakazi vimetangaza kusitisha Mgomo ulioanza Juni 3, 2024 baada ya Serikali kufanya mabadiliko kidogo ya Kima cha Chini cha Mishahara kutoka Tsh. 52,200 hadi Tsh. 104,400.
Licha ya usitishwaji wa Mgomo huo ulioripotiwa kuathiri huduma muhimu kwa muda, bado kiwango kilichoongezwa hakijafikia matakwa ya Wafanyakazi ambao walitaka Kima cha Chini kiwe kati ya Tsh. 800,00 hadi Tsh. 900,000.
Baadhi ya shughuli zilizoathiriwa na Mgomo huo ni pamoja kuzimwa kwa Gridi ya Taifa ya Umeme, Kufungwa kwa Shule, Kusimama kwa Huduma za Hospitali, Benki na Kusitishwa kwa Safari za Ndege.
Ni mara ya 4 kwa Migomo kutokea nchini humo tangu Rais Bola Tinubu alipochaguliwa kuongoza Taifa hilo linaloripotiwa kukabiliwa na mgogoro wa Kiuchumi huku thamani ya Fedha yake ikiendelea kushuka dhidi ya Dola