Nigeria huenda ikapiga marufuku shahada kutoka kenya na uganda

Kenya na Uganda huenda zikaongezwa katika orodha ya nchi ambazo shahada zao vya vyuo vikuu hazitambuliwi Nigeria.

Hayo yanajiri siku chache baada ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kusitisha kuzitambua shahada kutoka Benin na Togo.

"Hatutaishia Benin na Togo pekee," Waziri wa Elimu, Tahir Mamman alisema Jumatano wakati wa mahojiano kwenye kituo cha Televisheni cha Nigeria.

"Tutaongeza nchi kama Uganda, Kenya, hata Niger," alieleza. Agizo hilo jipya ni juhudi za kukomesha udanganyifu kutoka vyuo vya kigeni, kufuatia ripoti ya gazeti la Daily Nigeria.

Katika uchunguzi wa siri, ripota wa gazeti hilo Umar Audu alifichua jinsi alivyopata shahada ya miaka minne kutoka chuo kikuu cha Benin chini ya miezi miwili.

Nigeria imeanzisha uchunguzi rasmi kuhusu wizara na mashirika yanayohusika na kuidhinisha vyeti vya masomo nje ya nchi.

Waziri Mamman amesema hatua hiyo italinda waajiri wa Nigeria na sifa za nchi hiyo.

Share: