Nashukuru sana msaada wa Marekani kwa ajili ya kuiangamiza Hamas na kuwarudisha mateka kiasi cha 140 waliobaki”, waliokamatwa na Hamas wakati wa shambulio lake la Oktoba 7 ambalo liliua watu 1,200 kusini mwa Israeli, kiongozi wa Israeli alisema.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza Jumanne kuwa ana uungaji mkono wa kikamilifu wa Marekani kwa taifa la kiyahudi kwa mashambulizi ya ardhini yanayoendelea huko Gaza dhidi ya wanamgambo wa Hamas, na wakati huo huo nchi hizo mbili zimeendelea kuwa imara dhidi ya wito wa kimataifa unaoongezeka wa kusitisha mapigano, katika vita vya Israel na Hamas.
“Nashukuru sana msaada wa Marekani kwa ajili ya kuiangamiza Hamas na kuwarudisha mateka kiasi cha 140 waliobaki”, waliokamatwa na Hamas wakati wa shambulio lake la Oktoba 7 ambalo liliua watu 1,200 kusini mwa Israeli, kiongozi wa Israeli alisema.
“Kufuatia mazungumzo mapana na Rais Joe Biden pamoja na timu yake, tulipokea uungaji mkono kamili kwa uvamizi wa ardhini na kuzuia shinikizo la kimataifa la kusimamisha vita”, Netanyahu alisema.
Lakini Netanyahu alikiri kwamba yeye na Biden hawakubaliani kuhusu “siku baada ya Hamas”, wakati vita vikimalizika. Natumai tutafikia makubaliano katika hilo pia, Netanyahu alisema.