Ndege ya Malaysia Airline iliyopotea 2014 kutafutwa tena kwa mara ya pili

Serikali ya Malaysia imekubali kuanzisha tena utafutaji wa mabaki ya ndege ya Malaysia Airlines MH370, iliyopotea zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Waziri wa Uchukuzi wa nchi hiyo, Anthony Loke amesema leo kwamba pendekezo la kutafuta eneo jipya katika Bahari ya Hindi Kusini lilitoka kwa kampuni ya uchunguzi ya Marekani, Ocean Infinity, ambayo iliitafuta ndege hiyo mpaka 2018.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilipotea ikiwa na abiria 239 mwezi Machi 2014 baada ya kukosa mawasiliano na udhibiti wa anga chini ya saa moja baada ya kupaa. Juhudi zamwanzoi za mataifa mbalimbali za kutafuta ndege hiyo zilikamilika mwaka 2017 baada ya miaka miwili ya kuitafuta bila mafanikio.

Waziri Loke ameweka makubaliano na Ocean Infinity kwa mkataba wa "hakuna kinachopatikana, hakuna malipo." Utafutaji mpya utajumuisha eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 15,000 katika Bahari ya Hindi kusini.

Share: