Ndege kubwa ya jeshi la qatar yawasili na misaada kwaajili ya watu wa hanang

Ndege kubwa ya jeshi la Qatar imewasilisha misaada ya vyakula na vitu vingine ambavyo vitapelekwa kwa wahanga wa maporomoko yaliyotokea mwezi Disemba 2023 na kuwaacha wengi bila makazi na vyakula.

Msaada huo umepokelewa na naibu waziri wa nchi,ofisi ya waziri mkuu sera, bunge na uratibu, Ummy Nderiananga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA ambaye amewahakikishia wahisani hao kuwa misaada itawafikia walengwa.

Akikabidhi misaada hiyo balozi wa Qatar nchini Tanzania Fahad Rashed Almarekhi amesema wameguswa kutoa msaada huo kwa watu wa Hanang kwani serikali ya nchi hiyo inatambua madhara makubwa ambayo waliyapata.

Share: