Nchi ya mexico imekatiza uhusiano na ecuador baada ya polisi kuvamia ubalozi wa mexico mjini quito

wameingia kwa nguvu" katika ubalozi huo katika "ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa

Mexico imekatiza uhusiano na Ecuador baada ya polisi kuvamia ubalozi wa Mexico mjini Quito ili kumkamata Makamu wa Rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas.

Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador alisema "wameingia kwa nguvu" katika ubalozi huo katika "ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa".

Glas alikimbilia katika ubalozi huo Desemba mwaka jana baada ya Ecuador kutoa hati ya kukamatwa kwake kwa tuhuma ya ufisadi.

Wakili wa Glas alisema hana hatia. Glas alihudumu kama makamu wa rais wa Ecuador kati ya 2013 na 2017.

Aliondolewa kazini kutokana na shutuma kadhaa za ufisadi dhidi yake.

Baadaye mwaka huo huo alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kuhusishwa na ufisadi katika kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil Odebrecht.

Waendesha mashtaka walisema alipokea dola milioni 13.5 za kimarekani kama hongo.

Aliachiwa kutoka gerezani Novemba mwaka jana lakini mamlaka ya Ecuador ikatoa hati nyingine ya kukamatwa kwa tuhuma zaidi ya rushwa, na kumfanya Bw Glas kutafuta hifadhi katika ubalozi wa Mexico.








Share: