Nchi tatu za ulaya zinatarajia kutambua uwepo wa taifa la palestina

Uchunguzi ndani ya jeshi la Israel unaendelea huku kukiwa na shutuma kimataifa.

Baadaye leo, nchi tatu za Ulaya, Ireland, Hispania na Norway, kutambua rasmi taifa la Palestina.

Tayari kuna watu wengi wanaounga mkono utaifa wa Palestina lakini matangazo haya matatu yataashiria mabadiliko makubwa barani Ulaya, ambapo utambuzi ni mdogo.

Haya yanajiri chini ya saa 48 baada ya raia wengi kuuawa katika shambulizi la anga karibu na mji wa Rafah huko Gaza, ambalo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelitaja kuwa "janga baya".

Uchunguzi ndani ya jeshi la Israel unaendelea huku kukiwa na shutuma kimataifa.

Mapigano yanaendelea karibu na Rafah, ambapo Netanyahu kwa mara nyingine tena ameahidi "ushindi", licha ya onyo kuhusu hatari ya vifo vya raia ikiwa operesheni ya kijeshi itaendelea.

Share: