Nancy gonzalez mtengenezaji wa mikoba ya kifahari amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kutengeneza mikoba yenye ngozi za wanyama pori

Mtengenezaji wa mikoba ya kifahari wa Colombia ambaye alikiri makosa ya kusafirisha mikoba iliyotengenezwa kwa ngozi za wanyama watambaao wanaohifadhiwa amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.

Nancy Gonzalez, ambaye ametengeneza mikoba iliyobebwa na waigizaji wa filamu ya Sex and the City na Britney Spears, alihukumiwa Jumatatu katika mahakama moja huko Miami.

Gonzalez, 71, alivunja mkataba wa kimataifa kwa kuingiza nchini kinyume cha sheria mikoba iliyotengenezwa kwa mamba na chatu.

Maafisa wanasema aliwasajili nchini Marekani kuleta mikoba hiyo.

Colombia na Marekani zote zimetia saini Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama na Mimea Walio Hatarini Kutoweka (CITES), ambao hulinda wanyama jamii ya mamba - na chatu, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Sheria ya Marekani.

Biashara ya mamba na chatu haijapigwa marufuku, lakini inadhibitiwa madhubuti chini ya sheria za mkataba huo.

Gonzalez hakuwahi kupata vibali muhimu vinavyohitajika na wadhibiti.













Share: