Hata hivyo, Serikali imesema Rais Hage ataendelea na shughuli zake za Urais pamoja na kuongoza Vikao vya Baraza la Mawaziri ambalo yeye ni Mwenyekiti wake. Ikumbukwe Namibia inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu Novemba 2024.
Serikali imeweka wazi taarifa za vipimo vya Afya vya Rais Hage Geingob (82) na kuueleza Umma kuwa kiongozi huyo amekutwa na Ugonjwa wa Saratani na anatarajiwa kuanza matibabu kama ambavyo Madaktari wake walivyoelekeza.
Taarifa ya Serikali imesema Rais huyo amekuwa akifanya vipimo vya afya mara kwa mara tangu aingie Madarakani mwaka 2014 ingawa Wananchi walianza kuhoji kuhusu uimara wa Afya yake kabla hata hajaingia Ikulu. Mwaka 2023 aliripotiwa kufanyiwa Upasuaji wa Mishipa ya Moyo.
Hata hivyo, Serikali imesema Rais Hage ataendelea na shughuli zake za Urais pamoja na kuongoza Vikao vya Baraza la Mawaziri ambalo yeye ni Mwenyekiti wake. Ikumbukwe Namibia inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu Novemba 2024.
Namibia imekuwa kati ya Nchi chache Barani Afrika ambazo hutoa taarifa kuhusu Afya za Viongozi wake ikiwa ni tofauti na Serikali za Nchi nyingi ambazo taarifa za hali za Kiafya za Viongozi huwa na Siri na kusababisha Umma kupatwa na taharuki za mara kwaa mara.