Nachingwea: zaidi ya mabinti 15,521 kupata chanjo ya dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi

serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa chanjo bure kwa mabinti wote

ZAIDI ya mabinti 15,521 wanatarajiwa kupata chanjo ya dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 9-14 katika Wilaya ya Nachingwea. 

Akizungumza wakati uzinduzi wa kampeni ya Chanjo dhidi Saratani ya mlango wa kizazi, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amesema kuwa mabinti wa Wilaya hiyo watapata chanjo wote kwa asilimia 100 ili kuokoa uhai wa mabinti hao.

Moyo amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa chanjo bure kwa mabinti wote ili kulinda afya za mabinti wote wa kitanzania.


Moyo amesema chanjo zinazotolewa ni chanjo salama haina madhara yoyote kwa mabinti na Serikali imekuwa inatoa chanjo salama hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuiweka jamii salama.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za Chanjo Wilaya ya Nachingwea Rehema Kuchukua amesema binti asipopata chanjo hiyo inakuwa hatari kwa maisha yake.

Share: