Mwanaharakati wa tanzania atunukiwa tuzo ujerumani

Mji wa Weimar umekuwa ukitowa tuzo hiyo ya haki za binaadamu kila tarehe 10 Disemba tangu mwaka 1995, ikiwa alama ya wajibu wake kufuatia uhalifu wa utawala wa Kinazi wa Ujerumani.

Mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binaadamu kutoka Tanzania, Joseph Moses Oleshangay, ametunukiwa Tuzo ya Haki za Binaadamu ya mji wa Weimar nchini Ujerumani.

Katika sherehe zilizofanyika jioni ya Jumapili (Disemba 10) mjini Weimar, Oleshangay alikabidhiwa tuzo hiyo yenye thamani ya euro 5,000 kwa kile ambacho watayarishaji walisema ni mchango wake kwenye kupigania haki za jamii ya Maasai, Kamatakamata ya raia Ngorongoro.

Oleshangay, ambaye mwenyewe ni kutoka kabila la Maasai, ni mjumbe wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu na amekuwa akitowa ushauri wa kisheria na kuweka kumbukumbu ya uvunjwaji wa haki za binaadamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mji wa Weimar umekuwa ukitowa tuzo hiyo ya haki za binaadamu kila tarehe 10 Disemba tangu mwaka 1995, ikiwa alama ya wajibu wake kufuatia uhalifu wa utawala wa Kinazi wa Ujerumani.

Share: