Musalia mudavadi: akanusha ripoti za kuwa kenya ina uhusiano mbaya na majirani zake

Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi, amekanusha ripoti za kuwa Kenya ina uhusiano mbaya na majirani zake, licha ya mizozo kadhaa iliyotokea hivi karibuni ambapo alisisitiza inatatuliwa Kidiplomasia.

Kenya inakabiliwa na kesi ya usambazaji wa mafuta na Uganda, pia Januari 16, 2024 ilimaliza mzozo wa usafiri wa anga na Tanzania. Januari 5, 2024 Sudan ilimrejesha nyumbani Balozi wake baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa Mohamed Dagalo (kiongozi wa vikosi vya wanamgambo wanaopigana na Serikali)

Aidha, Desemba 17, 2023, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pia ilimrejesha nyumbani Balozi wake wa Nchini Kenya baada ya muungano mpya wa waasi wa Kikongo wakiwemo M23 kuundwa Jijini Nairobi

Share: