
Staa wa filamu za mapigano, Jackie Chan, amethibitisha nia yake ya kuchangia utajiri wake wote, unaokadiriwa kuwa dola milioni 400, kwa ajili ya shughuli za hisani badala ya kumuachia mwanaye, Jaycee.
Jackie Chan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii, alianzisha Jackie Chan Charitable Foundation mwaka 1988. Taasisi hiyo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali kama elimu na misaada ya maafa.
Jackie Chan anaamini kuwa utajiri unapaswa kutumika kusaidia watu wengi zaidi na si kurithishwa. Msanii huyo ameweka wazi kuwa lengo lake ni kuacha alama ya kusaidia walio katika uhitaji duniani kwani historia yake inaanzia huko.
Je, unafikiri uamuzi wake ni wa busara? Tushirikishe maoni yako.
Share: