Muigizaji Danzel Washington ameokoka na kubatizwa na kaanza mafunzo ya utumishi

Denzel Washington mwigizaji mashuhuri wa Hollywood, amechukua hatua kubwa katika safari yake ya kiroho kwa kubatizwa katika kwenye kanisa la Kelly Temple Church of God in Christ (COGIC) jijini New York. Tukio hili pia liliambatana rasmi na kupokea leseni yake ya huduma ya injili.

Akiwa amelelewa katika familia yenye misingi thabiti ya Kikristo, ambapo baba yake alikuwa mchungaji wa Kipentekoste, imani ya Denzel Washington imekuwa sehemu muhimu ya maisha yake tangu utotoni. Hata hivyo, safari yake ya kiroho imeimarika zaidi miaka kadhaa ilivyopita, na sasa ni mshirika wa West Angeles Church of God in Christ huko Los Angeles.

Akizungumzia ubatizo huo, Washington aliutaja kama “mafanikio makubwa zaidi” katika maisha yake. Alitoa ujumbe wa kugusa moyo kwa waumini waliokuwepo akisema, “Ikiwa Mungu ameweza kufanya haya kwangu, hakuna lisilowezekana kwa mtu yeyote. Mbingu ndio kikomo pekee.”

Ubatizo huu umezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo baadhi walipongeza uchaguzi wa kanisa dogo kwa tukio hili kubwa, huku wengine wakijadili haraka ya kuingiza watu maarufu kwenye huduma za injili.



Safari hii mpya ya kiroho ya Denzel Washington inaonyesha nguvu ya mabadiliko ya kiimani na jinsi imani inavyoweza kugusa maisha ya watu wa tabaka mbalimbali. Kwa hatua hii, Washington amekuwa sio tu nyota wa Hollywood bali pia kiongozi wa kiroho anayevutia wengi kwa mfano wake.

Share: