Rafiki wa zamani wa A$AP Rocky anatazamiwa kutoa ushahidi kuhusu wakati ambapo nyota huyo wa muziki wa hip-hop anadaiwa kumfyatulia bunduki kwenye mtaa wa Hollywood mwaka 2021.
Rapper huyo alikataa mashtaka ya makosa mawili ya mashambulizi kwa kutumia silaha ya moto ya moja kwa moja.
Kwa mujibu wa #IndependentUK, video iliyowasilishwa kama ushahidi na upande wa mashtaka ilionyesha ugomvi wa kimwili kati ya wanaume wawili, huku wawili wengine wakingilia kati, wakati mmoja wao aliyevaa koti jeusi, ambaye upande wa mashtaka alimtambulisha kama Rakim Mayers (Asap Rocky), alitoa bunduki na kuielekezea, lakini hakufyatua risasi.
Hata hivyo, wakili wa utetezi wa Rakim alieleza kuwa Ephron alimuandama kwa sababu alijua kuwa ilikuwa ni bunduki ya bandia na kwamba Ephron ndiye aliyekuwa na uchokozi.
Vyanzo vinaarifu kuwa kesi hii inakuja baada ya rapper huyo mwenye umri wa miaka 36 kukataa pendekezo la mwisho la upande wa mashtaka kumlazimisha kukiri kosa moja kati ya mashitaka yake mawili ya uhalifu na kutumikia kifungo cha siku 180 jela na miaka mitatu ya majaribio. Hata hivyo, Mayers anasisitiza kuwa yeye ni msafi katika kesi hii.
iIkiwa atapatikana na hatia A$AP Rocky anaweza kukumbana na kifungo cha hadi miaka 24 jela. Kesi hii inatarajiwa kudumu kwa wiki tatu.