Morogoro: zaidi ya wanafunzi 10,000 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hawajaripoti

Zaidi ya Wanafunzi 10,000 waliochaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Kwanza katika Shule za Sekondari za Serikali mkoani humo hawajaripoti na kufanyiwa Usajili hadi kufikia Februari 2024. 

Akitoa taarifa hiyo mbele ya Kamati ya Ushauri, Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa, Hildegard Saganda amesema idadi hiyo ni kati ya Wanafunzi 56,827 waliochaguliwa. 

Aidha, hadi kipindi hicho, Halmashauri ya Kilosa na Manispaa ya Morogoro zimetajwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya Wanafunzi wasioripoti Shule

Share: