Mmoja kati ya wafanyakazi wawili wa kenya airways waliokamatwa na kushikiliwa mwezi uliopita ameachiliwa

Kukamatwa kwa wafanyakazi hao wawili kulilazimu Kenya Airways (KQ) kutangaza kwamba ilikuwa inasitisha safari za ndege kwenda mji mkuu wa Congo, Kinshasa, tarehe 29 Aprili.

Mmoja kati ya wafanyakazi wawili wa Kenya Airways waliokamatwa na kushikiliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita ameachiliwa, afisa mkuu wa Kenya Airways alisema Jumatatu.

Kukamatwa kwa wafanyakazi hao wawili kulilazimu Kenya Airways (KQ) kutangaza kwamba ilikuwa inasitisha safari za ndege kwenda mji mkuu wa Congo, Kinshasa, tarehe 29 Aprili.

"Nina shukrani kubwa kutangaza kwamba Lydia Mbotela, Meneja wa KQ nchini DRC, ameachiliwa hivi punde na mamlaka huko Kinshasa," Korir Sing'oei, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, alisema kwenye X.

Hakutoa taarifa kuhusu hatima ya mtu wa pili aliyekamatwa.

Share: