Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambaye pia ni Mwenyeji wa Sherehe za Siku ya Wafanyakazi kwa Mwaka huu 2024 akiwapokea viongozi mbalimbali wa Kitaifa wanaohudhuria Sherehe za Mei Mosi ambazo kwa Mwaka huu zinafanyika katika Viwanja vya Michezo vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho haya ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ujumbe wa Mwaka huu unasema "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na Kinga dhidi ya Hali ngumu ya Maisha"