Kwa Mrombo kata ya Muriet, miongoni mwa maeneo yanayokuwa kwa kasi jijini Arusha, hapa kwa kawaida ni hekaheka na pilikapilika za kila aina ikiwemo biashara ya uuzaji wa nyama ya mbuzi na vinywaji mbalimbali.
Mamia ya vijana wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa mbuzi choma eneo hili la kwa Mrombo na wateja tuliowakuta hapa wanazo taarifa za kuripoti kazini kwa Mkuu wao mpya Mh. Paul Makonda na wakazi wa mkoa wa arusha wanasema watashiriki katika mapokezi yake, kama ishara ya kuahidi kushirikiana nae kwenye majukumu yake mapya.
Kulingana na ratiba, Mkuu wa mkoa Mh. Paul Christian Makonda anatarajiwa kuripoti Arusha jumatatu hii ya aprili 8, 2024 tayari kuanza majukumu yake kwenye mkoa huu wa kaskazini mwa Tanzania.
Share: