Mkuu wa majeshi nchini kenya francis omondi ogolla aliagiza azikwe ndani ya saa 72 baada ya kifo chake

Mkuu wa majeshi nchini Kenya Francis Omondi Ogolla alivyoomba mazishi yake yatekelezwe.

Ogolla, ambaye alifariki wakati helikopta yake ilipoanguka muda mfupi baada ya kuruka siku ya Alhamisi, atazikwa nyuma ya nyumba yake, Siaya, Magahribi mwa Kenya.

Kwa mujibu wa familia yake, ikiwakilishwa na kaka yake, Canon Hezekiah Oduor, Mkuu wa Majeshi aliiomba mazishi yake yafanyike kwa wepesi bila kuletea gharama kubwa familia yake.

Ameagiza pia azikwe ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.

Ogolla ameomba asizikwe ndani ya jeneza, na badala yake afungwe kwa shuka mfano Waislamu wanavyovishwa sanda.





Share: