Mkuu wa majeshi nchini kenya francis ogolla amefariki dunia

Baadhi ya vyombo kuu vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa Mkuu wa Majeshi, Francis Ogolla ameaga dunia.


Taarifa zaidi kutoka vyanzo tofauti zinasema kuwa Mkuu huyo wa Majeshi, alikuwa akisafiri pamoja na abiria wengine ambao hawajatambuliwa, walihusika kwenye ajali ya Helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Kenya alasiri hii katika Kaunti ya Elgeyo-Marakwet, Bonde la Ufa.

Aidha, Msemaji wa Ikulu ya Kenya Hussein Mohamed amesema kuwa Baraza la Usalama la Kitaifa nchini humo likiongozwa na rais William Ruto limejumuika kwa mkutano wa dharura katika Ikulu ya Nairobi jioni hii.

Share: