Mkuu wa jeshi la polisi kenya inspekta jenerali (ig)  japhet koome amejiuzulu

Kufuatia kujiuzulu kwa IG Japhet Koome, Rais Ruto amefanya mabadiliko katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi

Mkuu wa Polisi Kenya, Inspekta Jenerali (IG), Japhet Koome amejiuzulu nafasi yake huku Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja akichukua nafasi ya Koome kama kaimu IG hadi msimamizi mkuu atakapoteuliwa na kuidhinishwa na Rais na Bunge la Kitaifa.


“Mhe. Rais William Ruto, mnamo tarehe 12 Julai 2024, amekubali kujiuzulu kwa Eng. Japheth N. Koome, MGH, kama Inspekta Jenerali wa Polisi Kitaifa,” imesema sehemu ya ujumbe Ikulu ya Nairobi.

Kufuatia kujiuzulu kwa IG Japhet Koome, Rais Ruto amefanya mabadiliko katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi ambapo amemteua Bw. Eliud Langat kuwa Kaimu Naibu Inspekta Jenerali, Huduma ya Polisi ya Kenya huku Bw James Kamau akiwa Kaimu Naibu Inspekta Jenerali, Utawala wa Huduma ya Polisi.

Share: