Pesa hizo zilitokea Libya wakati wa utawala wa Muammar Gaddafi
Mke wa Rais wa zamani wa Ufaransa Bi. Carla Bruni-Sarkozy (56), ameshtakiwa kwa kuingilia ushahidi dhidi ya kesi inayomkabili mume wake.
Rais Mstaafu Nicolas Sarkozy (69), anatuhumiwa kupokea Mamilioni ya fedha kwa ajili ya kampeni kinyume na sheria.
Pesa hizo zilitokea Libya wakati wa utawala wa Muammar Gaddafi.
Pamoja na kuingilia ushahidi kupitia mtu aliyeibua tuhuma hizo, Bi.Sarkozy pia ameshtakiwa kwa kuwahadaa Mahakimu.
Mwanamama huyo yuko nje kwa dhamana na amepigwa marufuku kuwasiliana na watu wote wanaohusika na kesi hiyo isipokuwa mumewe tu.
Rais Mstaafu Sarkozy alifunga ndoa na mwanamuziki huyo ambaye pia ni mwanamitindo wa zamani, mnamo mwaka 2008 wakati akiwa Madarakani.