Mkataba wa montreal waliepusha shirika la ndege qatar airways kushtakiwa nchini australia

Wanawake watano wa Australia ambao walivuliwa nguo na kukaguliwa katika uwanja wa ndege wa Doha wameshindwa katika azma yao ya kulishtaki shirika la ndege la Qatar Airways.

Wanawake hao na wengine waliamriwa kuondoka kwenye ndege na kukaguliwa ikiwa walikuwa wamejifungua baada ya mtoto kupatikana ametelekezwa kwenye pipa la uwanja wa ndege mnamo 2020.

Tukio hilo lilisababisha hasira kwa umma na lilishutumiwa na mataifa kadhaa.

Mahakama ya Australia iligundua kuwa shirika la ndege la serikali lilikuwa na kinga dhidi ya mashtaka ya nchi ya kigeni.

Wanawake hao watano waliwasilisha madai katika Mahakama ya Australia mwaka wa 2021, wakitaka kulipwa fidia kutokana na madai ya "kugusana kinyume cha sheria" na kifungo kinyume cha sheria, ambacho kilisababisha athari za afya ya akili ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo na tatizo la mfadhaiko.

Abiria wengine - ikiwa ni pamoja na kutoka Uingereza na New Zealand - hawakuwa sehemu ya kesi hiyo.

Lakini siku ya Jumatano, Jaji John Halley aligundua kuwa sheria zinazosimamia usafiri wa kimataifa zilimaanisha Qatar Airways na mdhibiti wa usafiri wa anga wa nchi hiyo hawezi kushtakiwa.

Aliashiria mkataba wa kimataifa unaoitwa Mkataba wa Montreal ambao unatumika kuweka dhima ya shirika la ndege katika tukio la kifo au majeraha kwa abiria.








Share: