Miezi miwili baada ya mkataba wa kihistoria wa makubaliano ya ulinzi wa somalia na uturuki yazaa matunda

Meli ya jeshi la wanamaji la Uturuki imewasili katika Bandari ya Mogadishu kufuatia kusainiwa kwa makubaliano ya ulinzi na uchumi kati ya Somalia na Uturuki mwezi Februari mwaka huu.

Kinaliada F514 ilitia nanga bandarini Jumanne, miezi miwili baada ya mkataba wa kihistoria uliosainiwa kati ya nchi hizo mbili, ambapo Uturuki ilikubali kuipa Somalia msaada wa usalama wa baharini.


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, mawaziri kadhaa, na balozi wa Uturuki nchini Somalia, Alper Aktas, walihudhuria sherehe ya kuwakaribisha.

Share: