Kuna uhusiano mkubwa kati ya Uchumi Hai na Mfumo wa Demokrasia wa Nchi
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Michael Battle anasema “Kwa sasa tuna Rais Samia, ametoa fursa ya uhuru wa Demokrasia, sio tu kuruhusu uhai wa Vyama Vingi, pia ameruhusu uhuru wa kujieleza kwa kiwango kikubwa, ikimaanisha Demokrasia imekua”
Amesema “Amefanya Watu wawe huru kuandamana hadi ndani ya Dar es Salaam, Watu wengi wamekuwa huru kuelezea hisia zao, sifa hizo siyo tu zinaenda kwa Serikali yake bali hata kwa chama kinachotawala”
Battle ameongeza “Kuna uhusiano mkubwa kati ya Uchumi Hai na Mfumo wa Demokrasia wa Nchi, mfano Jakata Kikwete, aliruhusu mabadiliko yenye fikra chanya na kuwapa fursa vijana, amezungumza nao na amewapa ushauri wa masuala mbalimbali”
Balozi Michael Battle anasema Tanzania ina bahati ya kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya Nchi na ndio maana wamekuwa wakiruhusu uwepo wa vyama vingi na kuruhusu ukuaji wa Demokrasia Nchini
Ameongeza “Hivi karibuni tulimpoteza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, moja kati ya sifa yake kubwa ni kuruhusu Soko Huria, kubadilisha Sera za Kiuchumi na mabadiliko ya Kiuchumi, japokuwa naye aliendeleza Msingi ambao ulishatengenezwa na Mtangulizi wake, Mwalimu Julius Nyerere.”
Amesema hayo wakati wa Kongamano la Majadiliano Rika (Intergenerational Dialogues) baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa katika Ukumbi wa Confucious, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Machi 11, 2024