Mhe. waziri gwajima amempongeza mhe. makonda kwa kuendelea kuyatambua na kuyawezesha makundi mbalimbali ya kijamii

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ofisini kwake mapema leo Mei 2, 2024.

Katika Mazungumzo yao, Mhe. Waziri Gwajima amempongeza Mhe. Makonda kwa kuendelea kuyatambua na kuyawezesha makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kundi la Vijana maarufu kama 'Wadudu' linalojishughulisha na shughuli mbalimbali za sanaa mkoani Arusha.


Mhe. Gwajima ni miongoni mwa Maafisa wa serikali waliohudhuria sherehe za Mei Mosi kwenye Viwanja vya Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na leo amekutana na Menejimenti ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru.

Share: