Mhe. samia suluhu hassan amefanya uteuzi wa mabalozi na wakurugenzi wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuivunja bodi hiyo kama ifuatavyo:

Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.

Amemteua Balozi Said Hussein Masssoro kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait. Balozi Masssoro anachukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amemteua Mheshimiwa Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC). Mheshimiwa Mkeyenge anachukua nafasi ya Dk Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi nyingine

Pia Amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 07 Novemba, 2023.

Share: