Mhe . kapinga: tgdc onesheni matokeo chanya kwa kuzalisha umeme

Kampuni ya Uendelezaji wa Joto Ardhi Tanzania (TGDC) imetakiwa kuonesha Matokeo Chanya kwa kuzalisha Umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotoardhi ili kuunga Mkono Mpango wa Serikali wa kuwa na Nishati Safi na Endelevu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo pamoja na Menejimenti ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukutana na baadhi ya Taasisi na Kampuni zilizo chini ya Wizara ya Nishati kwa lengo la kuona Utendaji kazi wa Taasisi hizo .

Mhe. Kapinga ameieleza TGDC kuwa wabunifu na kutumia uwezo wao wote kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo inaanza kuzalisha umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotordhi kwa kuwa tayari baadhi ya maandalizi yameshafanyika katika maeneo ya vipaumbele.

Amesema kama ambavyo Serikali imejipambanua kuwa inatekeleza Mpango wa Nishati Safi na Endelevu, ni wakati wa TGDC sasa kuonesha uwezo wao katika kufanikisha hilo ili kutoa mchango mkubwa kwa Taifa. 

Vilevile amewasisitiza kuwa ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya na ya haraka zaidi ni vyema wakaongeza ubunifu, uthubutu, kushirikiana na kutoridhika na kila wanachofanya ili kupiga hatua mbele zaidi. Hali hiyo itaondoa changamoto ya umeme unayoikumba nchi kwa kuzingatia kuwa nishati ya Jotoardhi ni endelevu.

Share: