Mhe. jerry silaa aendesha msako wa kukamata watu kadha ambao wanatuhumiwa na wananchi kwa kusababisha migogoro ya ardhi

Kwa mujibu wa Waziri Silaa eneo hilo limekuwa likizuwa taharuki kwa wananchi ambao wameuziwa viwanja kinyemela na watu hao

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameagiza kukamtwa kwa watu kadha ambao wanatuhumiwa na wananchi kwa kusababisha migogoro ya ardhi na kuuza maeneo kinyume na taratibu kwa wakazi wa Mbondole kata ya Msongola wilaya ya Ilala jijini Dar Es Salaam.

Waziri Silaa ametoa maagizo ya kukamatwa watu hao wakati alipofanya ziara katika eneo hilo linalomilikiwa na Taasisi ya Green foundation tangu mwaka 2017. 

Kwa mujibu wa Waziri Silaa eneo hilo limekuwa likizuwa taharuki kwa wananchi ambao wameuziwa viwanja kinyemela na watu hao waliovamia mali ya Green foundation ambao ndio wenye nyaraka za umiliki wa eneo hilo

Share: