Katika Mkutano huo Mhe. Makamba ameongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaaban
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) anashiriki Mkutano wa 45 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika nchini Ghana tarehe 18-19 Julai 2024.
Mkutano huu unaangazia masuala ya kiutendaji ya Umoja huo, unajadili ajenda muhimu kuhusu utekelezaji wa Dira ya AU ya 2063 katika kukuza umoja na mshikamano pamoja na kupitisha bajeti ya AU kwa mwaka 2025.
Katika Mkutano huo Mhe. Makamba ameongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaaban, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika Mhe. Innocent Shiyo na Mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.