Mhandisi mkama bwire ameteuliwa kushika nafasi ya kaimu afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira dar es salaaam (dawasa)

Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika leo June 03, 2024 Ofisi za DAWASA Jijini Dar es salaam.

Mhandisi Bwire ni Mtumishi wa Wizara ya Maji ambaye amehudumu kama Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Kibaha, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) na hadi anapokea jukumu hili alikuwa ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Uteuzi wa Bwire unakuja baada ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kumtaka aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiunga Kingu, akae pembeni ya majukumu yake kwa muda, kuanzia June 30,2024 na akatangaza kuiweka DAWASA chini ya uangalizi maalum wa Wizara ya Maji ili kuboresha utendaji wake kufuatia uzembe uliopelekea visima kukosa maji na kufanya Wakazi wa Dar es salaam kukosa maji.



Share: