Hatua hiyo inaimarisha umoja wa upinzani katika jitihada za kumshinda rais anayemaliza muda wake Felix Tshisekedi.
Mgombea wa nne katika uchaguzi wa rais wa mwezi huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , ametangaza hapo jana kujiondoa na kumuunga mkono Moise Katumbi.
Hatua hiyo inaimarisha umoja wa upinzani katika jitihada za kumshinda rais anayemaliza muda wake Felix Tshisekedi.
Delly Sesanga, wakili na mbunge wa jimbo la Kasai ya Kati na kiongozi wa chama cha Envol, ametangaza pia kumuunga mkono Katumbi, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la kusini mwa Katanga lenye utajiri wa madini.
Kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni mwezi uliopita, baadhi ya wagombea 26 walikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho, lakini waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo na wagombea wawili ambao sio maarufu wamejiondoa na kumuunga mkono Katumbi. Uchaguzi wa rais nchini Kongo utafanyika Desemba 20 mwaka huu.