Mgombea wa nne wa jamhuri ya kidemokrasia ya kongo amuunga mkono aliyekuwa gavana wa urais

Mgombea wa nne amejiondoa katika kampeni ya urais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kumuunga mkono aliyekuwa gavana na mgombea wa upinzani Moïse Katumbi.

Kwa kujiondoa kwa Delly Sesanga - mwanasheria na mbunge kutoka jimbo la Kasai-Kati - sasa kuna wagombea 21 wa upinzani wanaowania nafasi hiyo ya juu.

Watashindana na Rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi ambaye anawania muhula wa pili madarakani.

Kujiondoa kwa Bw Sesanga kunaonekana kuimarisha umoja wa upinzani baada ya waziri mkuu wa zamani Matata Ponyo na wagombeaji wengine wawili, Seth Kikuni na Franck Diongo, hapo awali, kumuidhinisha Bw Katumbi.

Kumekuwa na majadiliano katika mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria kwa lengo la kumchagua mgombea mmoja wa upinzani kukabiliana na Bw Tshisekedi, ambayo yalimalizika tarehe 17 Novemba bila kuafikiana.

Kampeni za uchaguzi zilianza wiki mbili zilizopita na kumalizika tarehe 18 Desemba - siku mbili kabla ya uchaguzi wa Desemba 20.

Kipindi cha kampeni tayari kimeshuhudia vifo, huku sita wakiuawa kwenye mkanyagano Jumamosi katika mkutano wa kampeni wa Bw Tshisekedi katika mji wa Mbanza-Ngungu magharibi.

Mapema Jumanne, mfuasi wa Bw Katumbi aliuawa kwenye maandamano huku kukiwa na makabiliano na wafuasi wa chama tawala katika jimbo la Maniema mashariki mwa nchi hiyo.

Share: