Meli nne za jeshi la wanamaji la urusi na manowari inayotumia nguvu za nyuklia na frigate zimewasili cuba

Meli hizo zimetia nanga kwenye Ghuba ya Havana - takriban maili 90 (km 145) kutoka jimbo la Marekani la Florida

Meli nne za jeshi la wanamaji la Urusi - ikiwa ni pamoja na manowari inayotumia nguvu za nyuklia na frigate - zimewasili Cuba, katika kile kinachoonekana kama kuonyesha ubabe huku kukiwa na mvutano na nchi za Magharibi kuhusu vita vya Ukraine.

Meli hizo zimetia nanga kwenye Ghuba ya Havana - takriban maili 90 (km 145) kutoka jimbo la Marekani la Florida.


Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema meli ya Admiral Gorshkov na nyambizi ya Kazan zinabeba silaha za hali ya juu, ikiwa ni pamoja na makombora ya hypersonic Zircon.

Hapo awali walifanya mazoezi ya makombora katika bahari ya Atlantiki.

Lakini wizara ya mambo ya nje ya Cuba inasema hakuna meli yoyote inayobeba silaha za nyuklia, na ziara yao ya siku tano haileti tishio kwa eneo hilo.

Maafisa wa Marekani wanasema wanafuatilia kwa karibu ziara hiyo.

Jeshi la Wanamaji la Marekani pia lilitumia ndege zisizo na rubani za baharini kuzuia meli za Urusi zilipokuwa zikikaribia Cuba, mshirika wa BBC wa Marekani CBS anaripoti

Share: