Meli iliyozama miaka 300 yagombaniwa na mataifa matatu

Kolombia mbioni kupata hazina kubwa kutoka kwenye meli ya Spanish galleon San José, iliyozama mnamo mwaka 1708 miaka 300 iliyopita karibu na pwani ya Cartagena, inayoaminika kuwa na thamani ya hadi dola bilioni 20

Meli hiyo iliyozama katika vita imekuwa katikati ya mvutano wa kisheria kati ya hispania, Colombia na taifa la Qhara Qhara, ambao wanadai hazina hiyo kama urithi wa mababu zao.

Operesheni hiyo kabambe ya uokoaji inalenga kupata tani 200 za dhahabu, fedha na zumaridi, huku Rais Petro wa Colombia akisisitiza umuhimu wake kama dhamira ya kitaifa kukamilika kabla ya muhula wake kukamilika.

Share: