Mbunge wa jimbo la vunjo dkt. charles kimei amehoji kutojengwa kwa kituo cha afya cha msae kutamfanya asirudi bungeni uchaguzi ujao

Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Dkt. Charles Kimei amehoji kutojengwa kwa kituo cha afya cha Msae, Mwika ambapo amedai kutokujengwa kwa kituo hicho kutasababisha asirudi bungeni baada ya uchaguzi ujao.

Dkt. Kimei amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alimuuliza kama ni kweli katika jimbo lake hakuna kituo kipya kilichojengwa ambapo Mbunge huyo alikiri vituo vya afya viwili vimejengwa.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange alimjibu Mbunge huyo kwa kumueleza kuwa Serikali inatambua kituo hicho ni chakavu na upo mpango wa kukarabati vituo vya afya chakavu baada ya kukamilisha ukarabati wa hospitali za halmashauri.

Share: