Mazungumzo na wataalamu wa tathimini ya uchumi sadc

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii licha ya kutokana na sera zake nzuri za kifedha na kiuchumi licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Dunia zikiwemo athari za Uviko 19 na mizozo ya kivita inayoendelea maeneo mbalimbali Duniani.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa licha ya changamoto za kiuchumi Duniani kote bado Tanzania iliendelea kuimarika ukilinganisha na nchi nyingine zinazoizunguka kutokana na uimara wa sekta ya kilimo, uchukuzi na ujenzi.

Aidha alieleza kuwa Tanzania inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya nishati ya umeme wa maji wa Julius Nyerere, mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Daraja la Kigongo – Busisi mkoani Mwanza ambayo kukamilika kwake kutachochea maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kuwa Tanzania imejielekeza pia katika maendeleo ya viwanda na kupeleka umeme vijijini ambapo takribani vijiji 1200 vimefikiwa, hatua itakayochochea uzalishaji viwandani na kuongeza mnyororo wa thamani.

Share: