Mawaziri wa mambo ya nje wa g7 wakutana tokyo

Mawaziri hao wa mahusiano ya kigeni wa G7 wanatarajia pia kujadili suala la mahusiano na Asia ya Kati yenye utajiri wa rasilimali

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili hii leo mjini Tokyo.

Viongozi wengine waliopo huko ni waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Analenna baerbock pamoja na ule wa Ufaransa Catherine Colonna ambaye amasema watajadili haja ya kujibu mahitaji ya raia huko Gaza na pia suala la kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu.

Mawaziri hao wa mahusiano ya kigeni wa G7 wanatarajia pia kujadili suala la mahusiano na Asia ya Kati yenye utajiri wa rasilimali, ushawishi wa China na kuandaa mazungumzo yajayo kati ya Rais Joe Biden wa Marekani na Xi Jinping wa China yanayotarajiwa huko San Francisco.

Share: