Matukio ya ubakaji nchini sudan imekuwa sehemu ya maisha

wahusika wakuu wanatokea pande zote mbili zinazopigana kuwania madaraka Jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka

Hala Al-Karib ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya SIHA inayojihusisha kutetea Haki za Wanawake Barani Afrika amesema Asilimia 70 ya matukio yaliyorekodiwa ya Unyanyasaji wa Kijinsia ni Ubakaji wa Magenge

Anasema hali hiyo imeongezeka hasa baada ya kuibuka kwa vita Aprili, 2023

Akizungumza na Kituo cha BBC, amesema wahusika wakuu wanatokea pande zote mbili zinazopigana kuwania madaraka Jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) lakini anadai Wanamgambo wa RSF wameitumia hiyo kama mbinu ya kutisha jamii.

Ameyasema hayo katika Kongamano linalofanyika Nairobi, Kenya kuangazia athari za vita Nchini Sudan kwa Wanawake.

Share: