Marekani yakataa muswada wa kuondoa wafanyakazi wake niger

Mswada huo wa sheria ulipingwa kwa kura 86 dhidi ya 11. Marekani mwezi huu ilitangaza rasmi kwamba kutokana na mapinduzi ya Niger, imesimamisha msaada, lakini maafisa wa Marekani, wamesema hakuna mpango wa kubasilisha uwepo wa wanajeshi wa Marekani, nchini humo.

Niger, imekuwa mshirika wa Wahington, katika kukabiliana na wanamgambo wenye msimamo mkali ambao wameua maelfu ya watu, la kukosesha makazi mamilioni zaidi barani Afrika.

Kuna wafanyakazi wa wizara ya ulinzi 1,000 ndani ya taifa hilo. Seneta wa Republikan, Rand Paul, ambaye aliwasilisha muswada, ametoa hoja kwamba wanajeshi hawakupelekwa kwa kufuata kanuni za Baraka za bunge, na kusema Wamarekani, hawapaswi kuwa hatarini katika mgogoro wa Niger

Share: