Marekani yaiwekea iran vikwazo zaidi

Marekani imeweka vikwazo vipya kwa mashirika 10 na watu wanne waliopo Iran, Malaysia, Hong Kong na Indonesia ambao inawashutumu kuunga mkono utengenezaji wa ndege zisizo na rubani za Iran, wizara ya fedha ya Marekani, imesema Jumanne.

Mtandao huo umewezesha ununuzi wa vifaa vyenye thamani ya maelfu ya dola kwa ajili ya shirika la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu, chini ya jeshi la anga na mpango wake wa ndege zisizo na rubani.

“Uzalishaji haramu wa Iran na kuenea kwa ndege zake hatari za UAV zisizo na rubani kwa washirika wake wa kigaidi Mashariki ya Kati na Russia, zimeendelea kuzidisha mivutano na migogoro pamoja na kudhoofisha uthabiti,” amesema Brian Nelson, waziri mdogo wa masuala ya ugaidi na upelelezi wa kifedha katika taarifa.

Washington kwa muda mrefu imekuwa ikiishutumu Tehran kwa kupeleka silaha hizo kwa Russia, na kutumika Ukraine.

Share: